Bregedia Jenerali Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Sharif Shekh. Othman, akizungumza na ndugu na jamaa wa marehemu kabla ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar jana.
Ndege ilichukuwa miili ya Askari wa JWTZ ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikitokea Dar-es-Salaam, tayari kwa mazishi yanayofanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
Ndugu na Jamaa wa marehemu wakiwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kupokea miili ya ndugu zao waliofarika katika jeshi la Kimataifa la kulinda Amaan Dafur nchini Siudan.
Wananchi wakiwa na Makamanda wa JWTZ kupokea miili ya Jamaa zao katika uwanja wa ndege wa Zanzibar , kwa kuwasili kwa miili hiyo ya marehemu kwa ajili ya maziko.
Mmoja wa Kizuka akiongozana na ndugu zake alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Dar kupokea mwili wa marehemu mume wake akifarijiwa na kuongozwa katika sehemu husika kwa ajili ya matayarishi ya mazishi .
Mmoja wa Kizuka akiongozana na ndugu zake alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Dar kupokea mwili wa marehemu mume wake akifarijiwa na kuongozwa katika sehemu husika kwa ajili ya matayarishi ya mazishi .
ukitizama hizi sura zao hawa watu waliouawa utaona hawakuwa na huruma wala nyuso za kawaida za kibinadamu , wana ukatili iliofichika katika mioyo yao kwa kuangali picha tu inatosha kusema walikuwa ni watu wa aina gani. Wamevuna walichopanda.
ReplyDeleteNadhani pia na wewe unakasoro kubwa mno. Huwezi kabisa kumuhukumu mtu kwa uzuri sura au ubaya na kumlinganisha na ubaya.
ReplyDeleteUfinyu wako wa akili ndio uliokuongoza kuandika utumbo huu.
Mimi nilibahatika kusoma na Shaibu, hakua mtu mbaya wala katili. Ni mcheshi na tafiki mzuri sana kwa kila mtu.
Mungu awasamehe walipokosea.