Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa UTPC
Wenyeviti Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania
Sekretariati ya UTPC
Wadau wa Habari
Tanzania
Mabibi na Mabwana,
Asalam aleykum, Tumsifu Yesu Kristu.
Leo ni mwaka mmoja
kamili tangu aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa
Iringa Daudi Mwangosi auawe pale kijiji cha Nyororo Mufindi wakati akiwa katika
kazi yake ya kuandika habari.
Familia yake na
ndugu zake, IPC, UTPC na wadau wengine hawawezi kamwe kusahau mauaji ya Daudi
Mwangosi kwani yalikua ni mauaji ya kinyama na ukatili wa hali ya juu.
Mpaka sasa hatujui
sababu zilizo pelekea Daudi Mwangosi kuuawa, lakini tunaamini kwamba kwamba
Serikali itafanya kila njia kuhakikisha wote waliohusika, hatua sitahiki
zinachukuliwa.
Zipo sababu nyingi za serikali kufanya hivyo
lakini kubwa ni kwamba:-
1. Niwajibu wa Serikali
kuwalinda raia wake wote bila kujali itikadi zao za dini, rangi, kabila au
siasa. Hivyo pale inapotokea raia wake ameua katika mazingira yasio ya kawaida
serikali inawajibu wa kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua wote
waliohusika. Kwa kufanya hivyo Serikali yetu itakua inatimiza wajibu wake wa
kuwalinda raia wake. Hivyo ndivyo utawala wa sheria unavyo taka.
2. Ndugu zangu wakati
tunaangahikia maisha ya duniani tukumbuke kwamba, kuna maisha mengine huko
Mbinguni ambako kila mmoja wetu atahesabiwa haki yake kulingana na matendo yake
hapa duniani. Hivyo hata aliyemuua Daudi Mwangosi ipo siku atakufa na
atawajibika kujibu kwanini alimua Daudi Mwangosi.
Tunaweza kushinda hapa duniani lakini kama hatutatenda
yale yampendezae Mungu hatuwezi kushinda mbinguni hata siku mmmoja.
Ndugu zangu nalisema
hili ili tukumbuke kwamba, hapa duniani tunapita tu na kama hapa tunapita ni
kazi bure kuasi na kutompendeza Mungu wetu kwani maisha yetu yote mwisho wake
uko huko.
Ninawaomba waandishi
wenzangu, kifo cha Mwangosi kitukumbushe kwamba kuna watu wasiopenda maendeleo
ya Tanzania au ya Watanzania ambao watafanya kila njia kuvuruga tasnia yetu kwa
kutumia njia zozote zile ikiwa ni pamoja na kupiga waandishi, kuua waandishi na
kufanya kila wawezalo ilimradi tu waandishi tusiweze kufanya kazi zetu vizuri.
Ninawaomba waandishi
wenzangu, kama waandishi tubaki kuwa sauti ya watu wote, wana siasa, na wasio
wanasiasa, wenye dini na wasio na dini, wenye nacho na wasio nacho, masikini na
matajiri sisi ni wa wote na nilazima tubaki hivyo. Katika kufanya kazi yetu hii
jamii lazima ituelewe hivyo. Tukiweza kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya
kazi yetu bila ya kuegemea upande wowote ule tutaifanya kazi yetu kuwa nyepesi
sana, Lakini lililo la muhimu sana kwa leo niwakumbushe ndugu zangu kuweka
USALAMA WETU MBELE KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE. KWANI HAKUNA HABARI YENYE
THAMANI SAWA NA UHAI WAKO.
UTPC kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali na Wafadhili tunajiandaa kuwajengeeni uwezo wa
kutathimini mazingira mnayofanyia kazi na hivyo kuweza kufanya uamuzi sahihi wa
namna ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Wakati tunajianda kufanya
haya, tukumbuke kwamba katika kila jambo tukiwa na balance na kufuata maadili, jamii
itasimama na sisi hata pale tutakapo onewa na wasio penda maaendeleo ya
Tanzania. Watu wanaodhani kwamba wanaweza kushinda duniani na mbinguni.
Mwisho tumuombe
ndugu yetu Daudi Mwangosi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.Amina
Kenny Simbaya
Rais UTPC
No comments:
Post a Comment