THE UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatatu,
Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne
ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa
Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun.
Mkutano huo wa siku mbili utafanyika
keshokutwa Jumatano na Alhamisi kwenye Ukumbi wa Queen Elizabeth 2 mjini
London.
Miongoni mwa mambo makuu ambayo mkutano huo
utazungumzia ni Serikali Uwazi na Ajenda ya Maendeleo Baada ya Mwaka 2015
wakati muongo wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) unafikia
mwisho.
Masuala mengine ambayo yatazungumzwa katika mkutano
ambao Rais Kikwete anaambatana na Mawaziri wake watatu ni pamoja na uwazi
katika manunuzi ya umma, uwazi katika mikataba, haki ya kupata habari, uwazi
katika ukaguzi wa fedha za umma, uwazi wa Serikali na vyombo vya habari, uwazi
katika mikataba ya maliasili, uwazi katika maendeleo ya nchi zinazoendelea.
Mawaziri wanaoambatana na Rais Kikwete katika
ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa
Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Mheshimiwa
Mwinyihaji Makame.
Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani
Jumamosi, Novemba 2, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
29
Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment