Mkurugenzi Mkuu wa wizara ya afya Zanzibar na Daktari Bingwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, amelazwa katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi baada ya kujeruhiwa vibaya na majambazi.
Dkt. Malik alikuwa Nairobi kikazi na alipotea tangu Ijumaa iliyopita na hakukuwa na mawasiliano nae, wahusika wa hoteli aliyofikia pia hawakuwa wakifahamu alipo mgeni wao.
Chanzo: Jamii Forums
No comments:
Post a Comment