Meneja wa Maabara ya Kampuni ya Usafishaji wa Mafuta ya ABS ya Ajman Bibi Farzana Waqar akimpatia darasa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake walipokuwa katika ziara ya kukagua maeneo huru ya uwekezaji Nchini Sharjah.

Mwenyekiti wa Kampuni ya huduma za Meli na usafishaji mafuta ya ALCO Bw. Syed Ijaz Hassan akimkaguza Balozi Seif na Ujumbe wake kwenye kara kana za Kampuni hiyo Mjini Ajman Nchini Sharjah.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na ujumbe wake akikagua harakati za ujenzi wa Bodi Mpya pamoja na matengenezo ya Meli kwenye chelezo kilichomondani ya eneo hujru la uwekezaji katika eneo la Hamriya Sharja.
Mwenyekiti wa uhifadhi wa mazingira ambae pia ni mshauri wa maendeleo ya ujenzi wa Mamlaka hiyo Dr. Mohammad Tariq akizungumza na Balozi Seif kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Maeneo huru ya Hamriya wakati wa mapumziko ya siara yao kwenye Mamlaka hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya maeneo huru ya uwekezaji ya Hamriya Nchini Sharja pamoja na Ujumbe aliofuatana nao.

Balozi Seif akibadilishana mawazo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Utengenezaji wa Nondo Bwana Islam Ally Saleh wakati walipokuwa wakitembelea kiwanda hicho kinachopata mali ghafi za kokoto kutoka Tanga Tanzania.
Balozi Seif akipand miti mbele ya jengo la Ofisi ya Kampuni ya Al – Khaleej ndani ya maeneo huru ya uwekezaji ya Hamriya Nchini Sharja kama ishara ya kumbu kumbu ya kutembelea eneo hilo la uchumi.

Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege pamoja na Bandari { HELIOEST GROUP } ulioongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Jean Marc Ciccotti katika Hoteli ya Pullman Mjini Dubai.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege pamoja na Bandari { HELIOEST GROUP } Bwana Jean Marc Ciccotti akibadilishana mawazo na Balozi Seif kuhusu sekta ya uwekezji katika Hoteli ya Pullman Mjini Dubai.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ


