Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus akionyesha eneo la juu la chumba cha chini ya bahari ambapo mgeni atapata fursa ya kupunga upepo pamoja na kuota jua.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus Maarufu “ Babu kwa Nini “akitoa maelezo ya hatua zilizochukuliwa kukamilisha ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari katika Hoteli ya Manta Resort iliyoko Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk na Naibu wake Mh. Bihindi Hamad.
Balozi Seif akiwa pembezoni mwa dirisha ndani ya chumba cha chini ya Bahari akiangalia samaki na mazingira yake mara baada ya kuuzindua mradi huo hapo Manta Resort Hoteli Makangale.
Balozi Seif akiangalia ngazi ya kutokea juu ya chumba cha chini ya Bahari katika Hoteli ya Manta Resort Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye sherehe za uzinduzi wa chumba hicho ikiwa ni muendelezo wa sherehe za kutimia miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.Pembezoni mwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Meneja Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus kwa kukamilisha ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari kwenye hoteli yake iliyopo Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba huku Waziri wa Habari Mh. Marouk akifurahia kitendo hicho.
Kitanda na mandhari halisi na nzuri iliyomo ndani ya chumba cha chini ya Bahari katika hoteli ya Manta Resort Makangale Kaskazini Pemba mradi uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif.
Sehemu ya choo katika chumba cha chini ya Bahari kilichopo kwenye Hoteli ya Manta Resort huko Makangale Pemba.
Mandhari nzuri ya Hoteli ya Manta Resort ya Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba eneo ambalo kipo chumba cha chini ya Bahari.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR)
No comments:
Post a Comment