Na
Kiza Sungura, MAELEZO
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa kilo 1,200 za mchele, lita 220 za mafuta
na mbuzi 25 kama zawadi yake ya krismasi
kwa makundi maalum.
Zawadi
hizo zilikabidhiwa jana na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo
kwa niaba ya Rais Kikwete katika hafla fupi iliyofanyika uwanja wa mahabusu ya watoto
jijini Dar es salaam.
Alisema
Rais Kikwete ametoa zawadi hiyo ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi
maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na
watato walioko katika mkinzano na sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania
wengine kusherekea sikukuu hiyo.
Alisema
mbali ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam , pia alitoa kwa makundi mengine
katika mikoa mbali mbali nchini.
Alisema
kwa upande wa Dar es Salaam
ametao msaada kwa vituo 11 vinavyosaidia huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza.
Vituo
vilivyofaidika ni kituo cha watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, makazi ya watoto
Kurasini, Temeke, makazi ya watoto yatima Msimbazi, kituo cha kwetu Mbagala, kituo
cha yatima na kituo cha chakuwama.
Vingine
ni mahabusu ya watoto, makazi ya watoto yatima Mburahati, kituo cha tuwapende watoto
Bunju, makazi ya wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe.
Alisema
kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam
zawadi zao watapatiwa katika maeneo yao .
Alivitaja
vituo vya nje ya Dar es Salaam kuwa ni kituo cha Mabaoni Chake Ckale Pemba, kituo
cha wazee Welezo Unguja, mahabusu ya wototo Moshi na makazi ya wazee
wasiojiweza Sukamaela Singida.
Vingine
ni makazi ya wasiojiweza Bukumbi na makazi ya wazee wasiojiweza Msufini, Tanga.
Alisema Rais ametoa zawadi hizo kwa kutambua
kuwa watoto na wazee wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika
kusherehekea sikukuu hiyo vyema.
No comments:
Post a Comment