Habari za Punde

Mchezo wa Kirafiki kusherehekea Miaka 50 ya Mapinduzi

Waaa uwanja wa Amaan ukiwa katika hali yake ya Enzi zile ukipendeza baada ya kufanyiwa ukarabarti mkubwa wa kuwekwa kwa nyasi bandia na kuwekwa kwa tata mpya na ile ya zamani kutolewa, ukirudi katika hali yake ya kiwango cha kimataifa na kurudisha heshima yake kati ya viwanja bora Afrika Mashariki  
Kampuni ya Azam Tv, imetowa zawadi kwa mfungaji bora katika mchezo wa kirafiki wa shamrashamra za Mapinduzi kutimia miaka 50, Zawadi hiyo imetolewa kwa Mfungaji wa bao la  kwanza katika mchezo huo kati ya Baraza la Wawakilishi na Timu ya Wizara ya Habari, Mchezaji wa Habari Amuor Nassor kuibuka mshindi wa Bao la miaka 50 ya Mapinduzi dhidi ya mchezo huo.  
Mchezaji wa timu ya Wizara ya Habari akijaribu kumpita beki wa timu ya Baraza la Wawakilishi, katika mchezo wa kirafiki wa kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Zanzinbar.Timu ya Wizara ya Habari imeshinda 4--1.
Beki wa timu ya Habari Ali Haji akimpita mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Ussi Jecha Simai, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Habari imeshinda 4--1 

        Wachezaji wajao wa michezo mbalimbali wakifuatilia mchezo wa kirafiki katika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mchezo huo uliofanyika uwanja wa Amaan, kutoka kushoto Bwa. Dau Hamad Meneja wa timu hiyo, Mhe, Mbarouk Mtando na Mhe. Nassor Salum Jazira, wakitafakari mchezo huo ili kuweza kushinda wakati ikiwa nyuma kwa mabao 3--1 
Mhe. Hamza Hassan akimpita beki wa timu ya Habari katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan,timu ya Habari imeshinda 4--1
Kocha wa timu ya Habari  Bwa Mzee, akitowa maelekezo kwa wachezaji wake katika mchezo wa kirafiki na timu ya Baraza la Wawakilishi uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Habari imeshinda 4--1  
Wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza kocha wao akitowa maelezo ya mchezo huo wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza wakati wakiwa wamefungwa mabao 2-1
Wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi wakiwa nje wakifuatilia mchezo wao na timu ya Habari kutoka  kushoto Mhe. Jaku Ismail, Mhe.Ali Abdalla na Mhe. Mohommed Salum Dimwa. 
    Mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Nassor Salim Jazira, akimpita beki wa timu ya Habari,
Mchezaji wa timu ya Habari Hiji Shajak akimpita beki wa timu ya Baraza katika mchezo huo wa kirafiki uiofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Habari imeshinda 4--1
           Mchezaji wa timu ya Baraza Mhe. Hamza Hassan , akiwapita wachezaji wa timu ya Habari
Meneja wa timu ya Baraza Dau Hamad akiwa na mpira katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan.
Beki wa timu ya Habari Ali Haji, akizuiya mpira na huku mchezaji wa timu ya Baraza Mbarouk Mtando, akijaribu kumzuiya katika mchezo huo. 

2 comments:

  1. hizo fedha za kukarabati huu uwanja kama zingetumika kuimarisha masuala ya maji si ingekuwa bora? visiwa vyetu havina maji ya kutosha kutwa tunatembea na madumu au kuvizia maji usiku wa manane , hivi ni kweli viongozi wetu wana akili timamu kutumia mamilioni kwa ajili ya starehe wakati kitu cha msingi ktk maisha ya binadamu kimetushinda? au ndio yale ya mlevi akipata mshahara lazima apitie kwa boraafya kwanza halafu ndio ajue habari za mke na watoto? akili si nywele kuna wengine wanazo na wengine hawana ,

    ReplyDelete
  2. waache majeshi wakauchezee gwaride, au ndo umetengenezwa kwa ajili ya sherehe za mapinduzi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.