Rais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati
wa Ibada maalum ya mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela iliofanyika kijijni kwao Qunu , Eastern
Cape , Afrika Kusini Desemba 15, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) kwa hotuba ya kusisimua
aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee
Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013.
Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais
Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi ya Mzee Madiba
ambapo Tanzania
ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini
mwa Afrika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni
wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi
Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu , Eastern
Cape , Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu
kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment