Habari za Punde

Dk.Shein Mgeni Rasmi katika Fensi Kibandamai​ti

 Wasanii wa fensi ambao hujipaka mafuta machafu (mobile) wakiwa na mishale  wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbnali na wananchi waliohudhuria kuangalia fensi hiyo iliyoshirikisha kazi za taasisi za Serikali na Binafsi,katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wasanii wa asili na vikundi vya ngoma wakati Fensi katika barabara ya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wengine waliokaa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
 Ngoma ya ndege ni miongoni mwa burudani za asili katika fensi zilizopita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiangalia Fensi iliyopita  katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Ngoma ya Beni (Mbwa kachoka)  ikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Aina mabali mbali za miti ya asili ikiwemo katika fensi, iliyopita katika Barabara ya  Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 
Kazi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zikioneshwa kwa wananchi mbali mbali waliofika kuangalia fensi katika barabara ya Kibandamaiti jana ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.