Habari za Punde

Rais Kikwete Aongoza Waombolezaji Kuuaga Mwili wa Goerg Liundi Karimjee Dar

 
 Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Goerg Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Goerg Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho
  Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu JGoerg Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo
 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakijumuika na waombolezaji  katika misa maalum ya kumuombea marehemu Goerg Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo

                                               Sehemu ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo.

 Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mmwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.