Habari za Punde

Zanzibar kuanzisha chuo cha mafunzo ya Amali kwa wanawake kwa kushirikiana na chuo cha Barefoot cha India

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi mara alipowasili katika Chuo cha Mafunzo ya Amali kiitwacho Tilonia,Wilaya ya  Ajmer  Jimbo la Rajastan akiwa  katika siku ya pili ya ziara yake Nchni India pamoja na Ujumbe aliofuatana nao
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) kwa niaba ta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini makubaliano  ya Uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw.Bunker Roy alitia saini (kulia) saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi Nchini India na ujumbe wake

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia)   akibadilishana hati za  makubaliano na  Bw.Bunker Roy baada ya kutiliana saini makubaliano  ya Uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na  Chuo cha Barefoot cha India, saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi Nchini India na ujumbe wake katika Eneo la Chuo Kijiji cha Tilonia Wilaya  ya Ajmer Jimbo la Rajastan India


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Bw.Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake katika Kijiji cha Tilonia  Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania  Debnath Shaw (kulia) baada ya Saini ya makubaliano ya uannzishwaji wa Chuo kama hicho Zanzibar..[Picha na Ramadhan Othamn,Ikulu.]No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.