Na
Kadama Malunde, ITILIMA
WAZIRI
Mkuu (mstaafu) Edward Lowasa, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya
mwanasiasa maarufu nchini ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Bariadi kupitia CCM, Edward Masanja Ng’wani aliyefariki dunia hivi karibuni.
Marehemu
ambaye ni miongoni mwa waasisi wa CCM amefariki dunia Aprili 13 wakati
akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo katika hospitali
ya Ocean Road
jijini Dar es Salaam.
Akitoa
salamu hizo kwa niaba ya Lowasa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis
Mgeja, alisema CCM imepoteza kiongozi shupavu ambaye mchango wake ulikuwa bado
unahitajika.
Katika
salamu zake kwa familia ya marehemu, Lowasa alisema alimfahamu marehemu kwa
miaka zaidi ya 35 iliyopita ambapo alifanya naye kazi za uongozi katika mkoa wa
Shinyanga wakati Lowasa akiwa Katibu msaidizi wa CCM mkoa huo.
“Ng’wani
alikuwa mwanachama na mwanasiasa mwaminifu, mkweli na jasiri katika kutetea
wananchi, hakika familia na wanaCCM mkoa wa Simiyu na kanda ya ziwa
wameondokewa na kiongozi shupavu,” alisema Lowasa katika salamu zake.
Aidha
alisema CCM itaendelea kukumbuka mchango wa marehemu kimawazo na ushauri wake
ndani ya chama na jamii kwa ujumla huku akiwataka wananchi kuendelea kumwombea
kwani chama na wanajamii walimpenda lakini mungu kampenda zaidi.
Aliiomba
familia ya marehemu kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Marehemu
Ng’wani alizaliwa 1935 katika kijiji cha Bunamhala katika wilaya ya Itilima
mkoa mpya wa Simiyu na mazishi yake yamefanyika katika kijiji alichozaliwa Aprili
18.
No comments:
Post a Comment