Na
Fatuma Kitima, DSM
IDADI
ya watu waliokufa kutokana na mvua imeongezeka kufikia 11, baada ya mtu mmoja mkazi wa Kimara, Suka
Golan, kukutwa akiwa amekufa katika eneo la Unyamwezini kati ya Makoka na
Kimara.
Kifo
hicho kinafanya idadi ya waliokufa kufikia 11 kutokana na mvua hizo.
Taarifa
kutoka kwa shuhuda wa tukio, Aman Shaban, alisema maiti ilionekana eneo hilo
majira ya saa 12:00 jana, ambapo mwili wake ulikutikana ukimwa umekwama kwenye
miti.
Alisema
baada ya kuona mwili huo, taarifa
ilitolewa kwa jeshi la polisi
ambapo baada ya muda mfupi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa
marehemu.
Mbali
ya vifo, mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ambapo daraja
la Makoka liliopo mpakani kwa Kinondoni na Ilala limebomoka na kusababisha huduma za usafiri kukwama.
Hali
hiyo inasababisha wananchi kulipa shilingi 500 kwa vijana waliopiga kambi
katika daraja hilo
kwa ajili ya kuwavusha watu.
Katika
tukio jingine magari takribani 35 ya kampuni ya usambazaji mabomba ya gesi yamesombwa
na maji katika eneo la Mzinga Mbagala jijini Dar es Salaam.
Taarifa
kutoka kwa mashuhuda kutoka eneo la tukio, zilisema magari hayo yanayomilikiwa
na Wachina, yalikokotwa na maji wakati yakiwa yameegeshwa.
Wakati
huohuo, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam, imetoa taarifa
kuhusu madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Taarifa
ya kamati hiyo ilisema mvua hizo zimesababisha vifo, nyumba kubomoka huku
nyumba nyingine zikiwa bado zimezingirwa ma maji.
Madaraja
takribani 11 yamesombwa na maji na mengine kuvunjika huku mengine yakiwa yamefunikwa kabisa likiwemo
daraja la mto Mpiji mpakani wa Mkoa wa
Dar es Salaam na Pwani katika barabara iendayo Bagamoyo ambalo kingo zake
upande wa Dar es Salaam zimesombwa na maji na kusababisha mawasiliano kati ya
Bagamoyo na Dar es Salaam kukatika.
Makamu
wa Rais, Dk. Mohammed Gharib, ametembelea eneo hilo kujionea uharibifu mkubwa uliosababishwa
na mvua.
Katika
maeneo ya Mlandizi, kumekuwa na foleni kubwa ya magari ya mikoani
iliyosababishwa na mafuriko katika mtu Ruvu.
Aidha,
daraja la Visiga liliopo kilimoita 35 kabla ya kuingilia Mlandizi limetitia na
malori hayaruhusiwi kupita na kusababisha mawasiliano ya barabara kati ya
Mlandizi na Chalinze kukatika.
No comments:
Post a Comment