Sekta ya utalii Tanzania
inakabiliwa na ukosefu wa utoaji huduma bora tatizo linalochangia upungufu wa
watalii wanaotembelea nchini ikilinganishwa na nchi za jirani.
Mkurugenzi
mtendaji wa Taasisi inayotoa huduma za Utalii Tanzania ya Travel port, Elisaph Mathew alisema miongoni mwa matatizo
hayo ni gharama na watendaji wasiokuwa na ujuzi hali aliyodai imesababisha
malamiko mengi ya wageni na kupunguza mapato.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya utoaji wa huduma za
sekta hiyo kwa njia ya Electronic amewataka wadau wa sekta hiyo kuacha
kufundisha watendaji wao kiholela ili kupata watendaji watakaofanya kazi kwa
ufanisi
Nae Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya kitalii ya Zenith Salim Mohamed Suleiman amesema Zanzibar
imepata nafasi nzuri katika kukuza sekta ya utalii na kufikia viwango vya
kimataifa.
Mafunzo hayo
utoaji wa huduma kwa njia ya elekrtonic ni ya kwanza zanzibar yametolewa
kupitia kampuni ya zenith kwa ushirikiano na kampuni ya Travel port yenye
matawi zaidi ya mia na hamsini duniani
HAO NI GALILEO BWANA.... WANAONGOZA KWA UBORA WA HUDUMA ZAO.
ReplyDeleteNA KAMA MTU ANAHITAJ KUFUNGUA KAMBUNI YA TRAVEL (AIR TICKTING) AWAFUATAE...
Thanks for a good news.