Na
Donald Martin
ASKOFU
wa jimbo Katoliki la Zanzibar, Augustino Shao, ameyataka makundi yanayokinzana
katika bunge maalum la katiba, kuachana na ubinafsi na itikadi za kisiasa ili
kufikia muafaka katika masuala muhimu.
Askofu
Shao alitoa rai hiyo katika ujumbe wa sikukuu ya Pasaka kwenye ibada ya misa ya
mkesha wa sikukuu hiyo, iliyofanyika katika kanisa la Minara miwili mjini Zanzibar .
"Sasa
tunashuhudia makundi yenye nguvu yakijaribu kushinikiza kuingizwa matakwa yao
kwenye katiba kwa njia zozote ili kuendelea kulinda maslahi yao ya kisiasa,"
alisema.
Aliwataka
wajumbe wa bunge hilo
kufanya kazi kwa uadilifu ili kufikia muafaka katika masuala muhimu
yatakayowahakikishia raia wa kawaida kushiriki kwenye fursa za maendeleo kwa
manufaa ya wote.
Alisema
ili kupata katiba bora hakuna kuiheshimu kazi ya Tume ya Mabadliko ya Katiba
pamoja na kuwa na nia njema ya kutafuta suluhisho la matatizo mengi ya utendaji
katika dola zilizopo katika Muungano.
"Chaguo
la muundo wa dola sharti liongozwe na
malengo na madhumuni ya umoja wetu wa kutaka tuishi kwa mshikamano. Muundo wa
serikal moja, mbili au tatu sharti ufanywe kwa dhamira safi ya kupata suluhisho
la matatizo ya Muungano," alisema.
Aliwapongeza
Rais Kikwete na Rais Shein kwa ujasiri wa kuamua kuanzisha mchakato wa kuandika
katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisheria na katika wakati
muafaka.
Wakati
huo huo, Francis Godwin kutoka Iringa anaripoti kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kilutheri (KKT) Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenburg Mdegela, amelaani vikali wale wote
wanaowatukana waasisi wa taifa, marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza
katika misa ya Pasaka, alisema watu hao wanapaswa kuwaomba radhi Watanzania huku akisisitiza wajumbe wa Umoja
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurejea bungeni au wafungashe virago na kurudi nyumbani.
Askofu
huyo ambae pia ni mjumbe wa bunge maalum la katiba, alisema Watanzania wanataka kuikataa lulu waliyopewa na Mungu lulu ya
amani na kuanza kutafuta kuvurugana.
"Kinachofanywa bungeni kwa
sasa ni mzaha wa hali ya juu na
Watanzania wanapaswa kuwachunguza
vyema wawakilishi wao hao wakiwemo
wabunge wa vyama vyote na wale wanaoeneza mbegu ya chuki,” alisema.
Asema
wajumbe wa bunge la katiba hawana sifa ya
kutengeneza katiba kwani
wametanguliza mzaha na matusi
yasiyo na tija na kwamba wanaokwepa
bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi
wanapaswa kuzuiwa na vyombo vya usalama .
"Kama
wamekula pesa za wananchi kwa muda wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje leo
watoke bungeni na kudai kwenda kwa wananchi mikono mitupu,” alihoji.
"Wananchi
tuwakatae wajumbe wanaotaka kuzunguka
kupandikiza chuki kwa kujiita wao wapo kwa ajili ya katiba ya wananchi ilhali wamekimbia bunge na kutaka kutuwakilisha nje ya bunge,” alisema.
Aliwataka Watanzania
kuyatazama mataifa jirani kama
Kenya ambao walijipenda wao na kushindwa kuwapenda
majirani sasa Wasomali
wameingia wanawasumbua.
Nae
Jumbe Ismailly kutoka Singida, ameripoti kwamba Askofu wa Kanisa la Miracle
Assemblies of God Ministry la mjini Singida, John Tesha, ametoa wito kwa Watanzania
kuchunga kauli zao wanazotoa katika kipindi hiki ambapo wajumbe wa bunge
maalumu la katiba wanaendelea na mchakato wa kujadili rasimu ya katiba.
Alitoa
wito huo kwenye hafla ya uzinduzi wa kanisa la Miracle Assembles of God
Ministry pamoja na kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa kanisa hilo, iliyokwenda
sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa skuli ya maandalizi ya kanisa hilo .
“Mimi nataka kutoa rai tu kwa Watanzania wote
na siyo kwa wale waliopo Bungeni pekee kuwa wajaribu kuelewa kwamba maneno
mengi siyo sababu ya kujenga nchi, bali wanatakiwa wachukulie neno la upendo
ili kujenga umoja,” alisema.
Alisema
kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakiishi katika hali ya amani, utulivu, upendo
na mshikamano kwa hivyo kanisa halitakuwa tayari kuona Watanzania wakivurugana,”
alisema.
“Unajua
chuki inapopandwa katikati ya jamii inaleta kufarakanisha watu lakini sisi
tunataka watu wapendane na wawe na amani ili tuendelee kujenga taifa bora,”
alisema.
Kwa
upande wake Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo, aliwaomba maaskofu na wachungaji kuongeza kasi ya kuwahubiria waumini wao ili
waweze kuona faida ya kuchangia katika masuala ya dini zao.
No comments:
Post a Comment