Habari za Punde

Norway na Zanzibar Zatiliana Saini ya Ujenzi wa Wodi Mpya ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Helse Bergen kiliopo Haukelang Norway Dkt. Stener Kvinnsland wakitia saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto eneo la Mnazi mmoja wakishuhudiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik.  
 Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik akizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya waliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi ya watoto eneo la Mnazi mmoja, utakaoghari bilioni moja na milioni mia sita za kitanzania mpaka kumalizika kwake.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik wakiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto Hospitali ya Mnazi mmoja.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.