Habari za Punde

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) na Jitihada za Kupambana na Umaskini Nchini.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao utasaidia kuwaongezea kipato.Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku 15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari (kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula  akisisitiza jambo kwa wasimamizi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja wakati wakitowa elimu ya kuibua miradi walipokuwa katika mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika 

Mmoja wa wawezeshaji wa Mpango wa kuwawezesha walengwa wa mpango wa PSSN katika kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia  ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja akisikiliza maelezo kutoka kwa walengwa wa mpango huo.

Afisa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Zanzibar,Bw. Abbas Salhe akitoa maelezo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini PSSN juu ya namna ya kuibua miradi ya PWP katika eneo la Shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja.

Afisa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Zanzibar,Bw. Abbas Salhe akitoa maelezo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini PSSN juu ya namna ya kuibua miradi ya PWP katika eneo la Shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja.


 Pichani walengwa wa PWP katika shehia ya Mpapa wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) juu ya namna ya uibuaji wa miradi kwenye eneo lao

Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika 

Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini wakisikiliza maelezo ya utaratibu wa kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji ,Unguja , kutoka kwa mwezeshaji wa Mpango huo (hayupo pichani).

Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B wakimsikiliza mwezashaji wa Mpango wa uibuaji wa miradi ya Ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za TASAF kuongeza kipato kwa walengwa ambao watapaswa kutumia nguvu kazi yao kuitekeleza miradi watakayoibua.
Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.