Habari za Punde

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ndugu Wanahabari,
 
Nina heshima kubwa kukuarifuni kuwa ZIRPP inakusudia kuitisha Mkutano wa Waandishi wa Habari kuzungumzia dhamira na malengo ya Kongomano kuhusu "Makutano ya Fikra" utakaofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 20 Juni 2014 saa 4.00 kamili za asubuhi katika Ofisi ya ZIRPP iliyopo nyuma ya Majestic Cinema, Vuga.
 
Chai, kahawa, vinywaji baridi na vitafunio vitatolewa kwa watakaohudhuria. Pia waraka mahsusi kuhusu Kongomano hilo utasambazwa kwa taarifa yenu zaidi.
 
Mahudhurio yenu yatathaminiwa sana.
 
Shukran.

Muhammad Yussuf
Mkurugenzi Mtendaji
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523
Zanzibar
TANZANIA
Tel: 0777 707820 Cellular
Tel: 0242 233526 Office
Email: yussufm@gmail.com
Weblog: www.zirppo.wordpress.com
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.