Habari za Punde

Sala ya Eid ul Fitr viwanja vya Maisara

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Baadhi ya Mashekhe na Viongozi wakijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] 
  Baadhi ya waislamu waliomaliza Swala ya Eid el Fitri wakimasikiliza Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed  (hayupo pichani ) alipokuwa akitoa Khutba baada ya swala hiyo ambapo aliwataka waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa upendo na mashirikiano katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
 Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed (aliyesimama) akitoa Khutba baada ya Swala ya  Eid el Fitri mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa na Wailslamu waliojumuika kwa pamoja katika viwanja  vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Watoto walioshiriki katika Swala ya Eid el Fitri na kuwatakia Kheri katika kusherehekea Sikukuu hii ya  kumaliza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.