Na Joseph Ngilisho,Arusha
MKWARE wa ngono jijini Arusha, (jina
linahifadhiwa) maarufu Boyoo(22) mkazi
wa Sombetini, amenusurika kipigo baada ya kubambwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka
15 anayesoma kidato cha tatu, skuli ya
sekondari ya Peace House.
Mtuhumiwa alikuwa amemuweka kinyuma
mwanafunzi huyo,huku wazazi wake wakiamini yupo masomoni.
Boyoo ambaye anamiliki studio ya kudurufu
kazi za wasanii ,anadaiwa amekuwa na
tabia ya kufanya ngono na vitoto vidogo na kuwabadilisha kama
nguo kwenye ‘geto’ lake.
Sekeseke la kubambwa kwa kijana huyo
lilitokea jana majira ya asubuhi baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo kupata
taarifa kuwa mtoto wao amewekwa kinyumba katika ‘geto’ la mtuhumiwa kwa muda wa
wiki moja huku familia yake ikiamini kwamba tayari yupo skuli akiendelea na
masomo yake.
Wazazi wa mwanafunzi huyo ambao ni wakazi
wa eneo la Unga Limitedi jijini
hapa,walifika katika ‘geto’ hilo na baada ya kugonga mlango , ndipo
walipokutana uso kwa uso na mtoto wao akiwa na kanga moja.
“Sisi tulijua mtoto yupo skuli lakini
tuliopata taarifa kuwa hayupo skuli na ndipo tulipofuatilia dereva bodaboda
aliyempakia siku hiyo na tulipomhoji vizuri huku tukimtishia kumpeleka polisi, alielekeza
mahala mtoto alipo na tulipokwenda tulimkuta,” alisema.
Baada ya mwanafunzi huyo b kukutana uso
kwa uso na wazazi wake,alianguka chini na kupoteza fahamu na alizinduka majira
ya mchana akiwa hospitali ya mkoa Mount
Meru alikokimbizwa kwa
matibabu.
Mwanafunzi huyo alikacha masomo tangu
Julai 28 mwaka huu na kuhamia kwa mtuhumiwa huyo huku akishindia chipsi na soda
na kusahau kwamba wazazi wake wamelipa ada ya shilingi 800,000 kwa ajili ya
kumsomesha.
Akizungumza huku akilia, mama mzazi wa
msichana huyo,Anna Martini,alisema mtoto wao alitoweka nyumbani siku ya Jmatatu Julai 28,baada ya wazazi wake kumfungashia
wakiamini anaenda skuli.
Alisema walipata taarifa kutoka uongozi
wa skuli hiyo kuwa mtoto wao hayupo na ndipo walipoanza kumsaka maeneo
mbalimbali na kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi cha Unga Limited.
Hatua zaidi zilichukuliwa kwa mtuhumiwa
huyo kupigwa pingu baada kukamatwa
kutokana na wazazi kutoa taarifa polisi.
Hata hivyo, wazazi wa mhuhumiwa walitaka
kulimaliza suala hilo
ili mtoto wao asifikishwe mahakamani kwa kufanya maelewano ya kuwapatia
fedha baadhi ya askari polisi.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha,
hakupatikana kuzungumzia suala hilo
baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Mwanafunzi huyo aliamuriwa kwenda kupimwa
ujauzito pamoja na maambukizi ya magonjwa ya kujamiiana.
No comments:
Post a Comment