Habari za Punde

Shaka ahutubia mkutano wa CCM Gombani kongwe, Pemba

 NAIBU Katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akisalimiana na aliekuwa mshika fedha kupitia jumuia ya vijana ya chama cha CUF jimbo la Wete Pemba Said Ubwa, muda mfupi mara baada ya kurejesha kadi ya chama hicho, na kujiunga na CCM, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)

WANACHAMA wa jumuia ya Vijana wa chama wa Mapinduzi ‘UVCCM’ wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kazi wa jumuia hiyo, mbele ya Naibu katibu mkuu wa jumuia hiyo Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)


NAIBU Katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wanachama wa jumuia ya CCM wa mikoa miwili ya Pemba, pamoja na wananchi wengine kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Gombani Kongwe kisiwani Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
KULIA ni Mkuu mpya wa wilaya ya Chakechake Hanuna Ibrahimu Massoud (aliekuwa afisa tawala mkoa wa kusini Pemba) akibadilishana mawazo na Mkuu mpya wa mkoa wa kusini Pemba (aliekuwa mkuu wa wilaya ya Chakechake) Mwanajuma Majid Abdallah wakati walipokutana kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na UVCCM kisiwani Pemba na kufanyika uwanja wa Gombani kongwe kisiwani humo (picha na Haji Nassor, Pemba)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.