Habari za Punde

Tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706

FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056

Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM

Tovuti: www.meteo.go.tz

Unapojibu tafadhali nakili:

Kumb. Na.: TMA/1622 31 Ogasti, 2014


Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani. Taarifa Na. 201408-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 6:00 Mchana
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
01 Septemba, 2014
Mpaka:
Tarehe
02 Septemba, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani.
Kiwango cha uhakika: Juu: (70%)
Maeneo yatakayoathirika Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maelezo: Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkali wa Kusi, mashariki mwa Pwani ya Tanzania.
Angalizo: Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.