Habari za Punde

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Afunga Michezo ya 8 ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Amaan Zanzibar.

Bendera ya Nchi Washiriki wa Michezo ya Nane ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zikipepea katika uwanja wa Amaan wakati wa ufungaji wa michuano hiyo iliomalizika leo Zanzibar, na Nchi ya Kenya kuibuka mshindi wa Jumla wa michuano hiyo ya 8 ya Majeshi. 
 Vikombe vilivyokabidhiwa kwa washindi wa Michezo ya majeshi yalioadhimishwa katika viwanja vya Amaan na kufungwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akimkabidhi Kombe la Ubingwa na Mpira wa Miguu Brigedia Jenerali wa Jeshi la Kenya Kabigu, baada tli yake kuibuka mshindi wa mpira wa miguu kwazifunga timu washiriki.

Waziri Mkuu Mhe. Mizingo Pinda akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Mhe. Hussein Mwinyi na katikati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Davis Mwamunyange, wakirudi kukagua timu za Tanzania na Uganda wakati wa ufungaji wa Michezo hiyo katika uwanja wa Amaan.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akisalimiana nahezaji wa timu ya Uganda wakati alipofika kuyafunga michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki uwanja wa Amaan Zanzibar.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akisalimiana nahezaji wa timu ya Tanzania wakati alipofika kuyafunga michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki uwanja wa Amaan Zanzibar.

Wakuu wa Majeshi wa Nchi za Afrika Mashariki wakitowa shaluti wakati wa kupigwa kwa wimbo wa Taifa wa Nchi ya Uganda na Tanzania wakati wa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda na Wakuu wa Majeshi wakisimama wakatin wa kupigwa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Uganda.
Wachezaji wa timu ya Jeshi Tanzania wakisalimiana na wachezaji wea Jeshi Uganda katika mchezo wao wa ufungaji wa michezo ya Majeshi katika mchezo wa mpira uliofanyika uwanja wa amaan, timu hizo zimetoka sare ya 1-1
Mchezaji wa timu ya Jeshi Tanzania akimpita beki wa timu ya Uganda katika mchezo wa kukamilisha michezo ya 8 ya Majeshi yaliofanyika Zanzibar. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
Mshambuliaji wa timu ya Jeshi Uganda akimpita beki wa timu ya Tanzania katika mchezo wao wa kufunga michezo ya Majeshi uliofanyika uwanja wa Amaan timu hizo zimetoka sare ya 1--1.
                    Wachezaji wa timu ya Uganda na Tanzania wakiwania mpira wakiwa chini











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.