Habari za Punde

Mahojiano na Ahmed Mngazija Muathirika wa madawa ya kulevya

Haya ni MAHOJIANO na Ahmed Mngazija a.k.a (Pongonyongo) jinsi alivyojiingiza bila ya kutegemea katika janga la madawa ya kulevya. 
Ahmed azungumzia mengi juu ya maisha ya wengi walioathirika na mihadarati kisiwani Zanzibar
Sikujua wala sikutambua lakini nilipomsikiliza kwa makini ndipo nilipofunguka na kuelewa zaidi juu ya ndugu zetu waliotumbukia bila ya kutegemea katika uvutaji wa madawa ya kelevya, na kwa kweli wanahitaji kupewa msaada mkubwa wa kuwaponyesha na majanga haya.
Jiunge nasi kwa kumsikiliza mwanzo hadi mwisho ili na wewe upate kujua nini kimejiri kwa Ahmed Mngazija.! Karibu kusikiliza nasi

3 comments:

  1. dah! inasikitisha sana kumbe pesa ya kuwapeleka huko soba ni hiyo tu laki 2, ndugu muandishi muandishi nahisi ungeweka kitu kama account ya mambo kama haya au kuchimba visima, mayatima nk ili watu wakapata kuchangia, au sijui kuna njia gani ya kuchangia na itakuwa vizuri kama itakuwa njia ya Paypal, mtu ukijisikia unabonya tu unashughulika mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Watu kama kina Maalim Seif au babu Juma Duni walikuwa sasahivi wamo serikalini wapigie debe hali za wafungwa, sababu washayaona wao, inawezekana ikawa bahati yako mbaya tu ukaishia jela sasa sio unateswa tena, hata pakulala mtihani?, wakati mwengine askari tu anataka kukutia adabu huna kosa lolote, ah lakini nchi za kidikteta ndo zinavokuwa mifano ipo tele.

    ReplyDelete
  3. Asante sana Anonymous wa kwanza ila tuna full information na pia Tunaomba msaada wa kuwasaidia hawa ndugu zetu ambao kwa sasa wamechoshwa na uvutaji wa madawa itapendeza sana ukitaka kumsaidia Aliehojiwa wasilina na Mimi kwa Email swahilivilla@gmail.com tutawafikishia ujumbe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.