Na Mwantanga Ame, Singida
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amesema hawatakubali kuona Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA), unauchafua
awamu ya pili ya mjadala wa kupatikana katiba mpya, kwani kamati 12 za bunge
zimemaliza kazi zake vizuri.
Aliysema hayo wakati
akiwahutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya
Chiuyu, wilaya ya Manyoni mkoaniSingida.
Balozi Seif, ambae pia ni Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alisema wanalazimika kutoa tahadhari hiyo kwa vile
tayari kuna taarifa kwamba umoja huo huenda ukarudi bungeni baada ya kuzungumza
na Rais Kikwete.
Alisema nafasi yao ya kurudi
isiwe sababu ya kuchafua awamu ya pili ya mjadala huo.
Alisma CCM itaendelea na
msimamo wake wa kutetea mfumo wa serikali mbili kwa sababu wananchi
wameshaelewa madhara ya mfumo wa serikali tatu.
Alisema inashangaza kuona
baadhi ya watu kudai wajumbe wa CCM, hawajadili rasimu ya Jaji Warioba, wakati
taratibu zinawaruhusu wajumbe kurekebisha palipokosewa.
Aidha alisema madai kuwa katiba
inayotungwa ni ya CCM hayana ukweli kwa sababu wajumbe wengine kutoka kundi la
201 wanashiriki kujadili.
Alisema nia ya serikali ni
kuona Tanzania inapata katiba iliyo bora na itakayowaunganisha wananchi.
No comments:
Post a Comment