Habari za Punde

Wazanzibari watakiwa kutunza amani iliyopo

WAZANZIBARI wametakiwa kuitunza amani iliyopo ndani ya nchi yao na kuondoa tofauti zao ndogo ndogo za mitazamo na za kimawazo ili kuepusha migongano itakayochafuwa jina zuri la Zanzibar.
 
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vijana Tanzania (TAYI) tawi la Zanzibar Bw. Abdallah Miraji katika hafla ya siku ya amaan duniani iliyofanyika huko kituoni kwao Mwembemadema mjini Unguja, ambayo husherehekewa kila ifikapo Septemba 21 ya kila mwaka.
 
Alisema kuwa Zanzibar wana tunu kubwa ya amani ambayo wapo watu wachache hawafurahii uwepo wake huo hivyo ni lazima kila mmoja wao awe askari katika kuilinda.
 
Alisema kuwa wazanzibari wana utamaduni wao wa kuvumiliana ambao unahitaji kuendelezwa na wakatae kabisa na kwa nguvu zao zote kupiga vita na kusema kuwa ndio kwa amani.
 
“Haya isiwe ni jambo la mzaha litoke ndani ya moyo na tulisimamie kwa dhati kabisa”, alisema.
 
Nae Katibu wa Jumuiya ya Amani, Ukweli na Uwazi Zanzibar (ZPTTA) Bw. Ali Mussa Mwadini amesema kuwa dunia imetoka katika wa amani na kuingia katika utamaduni wa vita jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa uchafuzi mkubwa wa amani.
 
Alisema kuwa pamoja na kutokea hayo lakini hakuwafanyi washindwe kusherehekea siku hiyo jambo la msingi ni kusisitiza amani  iendelee ili kuinusuru dunia kuwepo katika machafuko.

1 comment:

  1. mambo hayo waelezeni kisonge yale mabago wanayoandika pale.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.