Habari za Punde

Breeking Newss Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein Amteua Mwanasheria Mkuu Zanzibar.


Mhe Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya  Kifungu 55(1)cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.     

6 comments:

  1. Congratulation, Allah akuongoze katika utendaji wako na akupe moyo wa kujiamni na kusimamia kazi zako kwa uwadilifu. Ameen

    ReplyDelete
  2. si muliambiwa ccm mumetaka watu wapige kura za wazi ili mupate kuwashughulikia watu watokupingeni mukakataa, sasa vipi?, mbona munawatia adabu watu kwa kutumia demokrasia yao?.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mabadilko ya kawaida katika utumishi wa UMMA....!

      Delete
  3. jambo la kujiuliza mbona ccm wa bara wanasema wanavyotaka, wameenda kinyume na mawazo ya chama mbona hakufukuzwa mtu? sisi Wazanzibari tuna nini?, pia tuliwasikia maraisi wetu kua watu wakatoe maoni yao bila ya woga sasa vipi kuhusu Mansoury, au ulikuwa mtego tu?

    ReplyDelete
  4. Huo ni uamuzi wa busara sana, Othman Masoud alionesha utovu mkubwa sana wa nidhamu uliokithiri kwa serikali. Sisi wengine tulijua hata kabla ya mchakato wa Katiba kuanza kuwa sio chaguo sahihi kwa nafasi ile ya AG. He behaves differently ndani na nje ya jamii!!!

    ReplyDelete
  5. NIkweli AGm asuma alikuwa sichaguo la srekali ya znz, kwakuwa serekali ya znz, imezoweya kuongozwa na wakwezi na wakulima wasio jua kusoma na kuandika,na wala wasio jua samani yamali iweje mtukama huyu alie elimika umuweka ndani ya makundi yenye akili za samaki awezekufanya naokazi ni vigumu ni bora alivyoacha

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.