Habari za Punde

Dk Shein amtumia salamu za rambirambi kwa kaimu Rais wa Zambia

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                       30 Oktoba, 2014
TAARIFA KWA VYOMBOVYA HABARI
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amempelekea, Kaimu Raia wa Zambia Bwana Guy Scott, Salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Micheal Sata kilichotokea hivi karibuni.
 
“Mimi na wananchi wa Zanzibar tunatambua mchango wa marehemu katika ukombozi wa nchi yake kutoka kwenye utawala wa kikoloni na daima tutamkumbuka marehemu kwa juhudi zake za dhati katika kupigania demokrasia na kuunga mkono harakati za kuleta utengamano katika nchi za Kusini wa Afrika” Dk. Shein amesema.
 
Katika salamuz ake hizo Dk. Shein amesema amepokea kwa mshituko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Bwana Satta ambaye aliingia madarakani tarehe 23 Septemba, 2011 na kufanya awe Rais wa tano wa nchi hiyo.
 
“Tunaungana na wananchi wa Zambia katika kuombeleza msiba wa kiongozi huyu mkubwa na tunatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu na ndugu zetu wananchi wa Zambia” Dk. Shein alieleza katika salamu hizo na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema poponi. AMIN
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.