Habari za Punde

Dk.Shein Ampongeza Rais Mpya wa Indonesia Mhe,Joko Widodo.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                          24 Oktoba, 2014
TAARIFA KWA VYOMBOVYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia Salamu za Pongezi Rais Mpya wa Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.
“Mimi na wananchi wa Zanzibar tunakupongeza pia kwa ushindi wako huo ambao umekufanya kuwa Rais wa kwanza wa Indonesia kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi” alisema Dk. Shein katika salamu hizo.
Dk. Shein alimueleza Rais Widodo kuwa inafurahisha kuona Zanzibar na Indonesia zimekuwa na ushirikiano mzuri na wa kihistoria hivyo matumaini yake ni kuona ushirikiano huo unadumishwa na unaimarishwa katika kipindi cha utawala wa Rais huyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemtakia Rais Joko Widodo heri na mafanikio mema katika kuiongoza nchi yake.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

                                               

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.