Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Afungua Mafunzo Elekezi ya Utumishi

 Mkurugenzi wa  Utawala na Rasilimali Watu Bw. Barnabas Ndunguru akimkaribisha  mgeni rasmi ambaye ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo Pichani) katika ufungaji wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Wizara.Hafla hiyo ilifanyika  hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akiongea na baadhi ya Watumishi wapya wa Wizara katika ufungaji wa mafunzo elekezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo aliwaasa kuwa na maadili katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga katikati akiongea na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Leonard Thadeo kulia na Mkurugenzi  wa Maendeleo ya  Utamaduni  Prof. Hermens Mwansoko kushoto mara baada ya kufunga mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Wizara

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.