Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zenj kuchangia Miswaada Iliowakilishwa


Mwakilishi wa jimbo la Mkwajuni Mhe Mbarouk Mtando akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa jimbo la Amaan, Mhe Fatma Mbarouk Said, wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa kikao cha asubuhi kikiendelea. 
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Mhe. Ismail Jussa akiingia katika jengo la baraza la wawakilishi kuhughuria kikao cha asubuhi cha baraza hilo linaloendelea kujadili miswada iliowakilishwa kuchangia ili kuipitisha kuwa sheria.
Mhe Waziri wa Ardh, Maji Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaban,na Waziri wa Biashara Mhe Nassor Mzrui wakinukuu michango ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wanaochangia katika miswada iliowakilisha katika kikao hicho wakati wac michango ikiendelea kutolewa na wajumbe.
Watendajhi wa Wizara ya ArdhiMaji Makaazi na Nishati wakifuatilia michango ikiwakilishwa kuchangia Shirika la Nyumba Zanzibar, iliokuwa ikichangia na katika mkutano huo wa baraza
Mhe Mwakilishi Hassan Omar Hamad akichangia mswadfa wa shirika la nyumba katika kikao hicho cha asubuhi 

Wajumbe wakisoma kwa kina mswada wa kuazishwa kwa shirika la nyumba zanzibar, wakati baadhi ya wajumbe wakiuchangia katika kikao hicho. 



Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakiripoti habari za baraza la wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia michango hiyo.




Waziri wa Ardhi Maji Makaazi na Nishati Mhe. Ramadhani Abdalla Shaban, akizungumza na Watendaji wakuu wa Wizara yake wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kupitishwa mswada wa shirika la nyumba zanzibar.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Zanzibar Mhe. Jussa Ismail, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Maakazi na Nishati Ndg Mustafa Aboud Jumbe wakiwa na kulia  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said wakimsikiliza Mwakilishi huyo wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kupitisha mswadwa wa Shirika la Nyumba Zanzibar. uliojadiliwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.