Habari za Punde

Nyumba aliyokuwa akikaa Sahaba 'Urwah bin Zubeir bin Awwaam




Hii ndiyo nyumba aliyokuwa akikaa Sahaba 'Urwah Bin Zubeir,  Allaah Amuwie radhi.

Nyumba hii ipo njiani kutokea Madina (Saudi Arabia) kuelekea Dhul Khulayfah (au Abyaar Ali kama kunavyojulikana) kiasi cha km 3.5 kutoka Msikiti wa Mtume Swalla Allaahu 'Alayhi Wasallam.
 
'Urwah ni mmoja wa Masahaba waliohama Makkah na kuhamia Madina ( Muhaajiriin). Ni mtoto wa Sahaba Zubeir bin 'Awwaam Allaah Amuwie radhi. Zubeir bin 'Awwaam  ni miongoni mwa Masahaba waliobashiriwa pepo na Mtume Swalla Allaahu 'alayhi wasallam. Mama yake ni Asmaa bint Abubakr Assiddiyq.

Ni miongoni mwa nyumba chache ambazo bado zimeweza kusimama na kama unavyoona katika picha na imo katika matengenezo ya kurekebisha kuta zilizoanguka.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.