Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na IGP Ernest Mangu wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri yaWatu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko
wa Rais Xi Jinping.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na maafisa wa
Ubalozi wa China nchini Tanzanioa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa
mwaliko wa Rais Xi Jinping.(Picha na Ikulu )
mwaliko wa Rais Xi Jinping.(Picha na Ikulu )
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete aanza ziara rasmi ya China
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumanne, Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya
Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara yake ya pili
nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Baada
ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Vietnam kwa
mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.
Wakati
wa ziara yake nchini China, Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana,
Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo matatu ya nchi hiyo, atafanya
mazungumzo na viongozi wakuu wa China, atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu
ya shughuli za maendeleo, atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika
sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania
na China.
Rais
Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Xi
Jinping; Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Watu wa China, Mheshimiwa Zhang Dejiang.
Rais
Kikwete pia atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya miradi ya maendeleo ya
Tanzania ambayo inasaidiwa ama inagharimiwa na fedha kutoka China na pia
atakutana kwa mazungumzo na wakuu wa taasisi muhimu zinazogharimia baadhi ya
miradi mikubwa ya maendeleo katika Tanzania zikiwamo China-Africa Development
Fund (CADB) na China Development Bank (CDB).
Akiwa
Beijing, Rais Kikwete atakutana na Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao
katika China, atafungua Mkutano wa Tatu wa Biashara na Uwekezaji kati ya
Tanzania na China na atazindua rasmi Kijiji cha Kiafrika.
Aidha,
Rais Kikwete atatunukiwa uprofesa wa heshima na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China
cha China Agricultural University na Chuo Kikuu cha East China Normal
University na pia atakuwa mwenyeji wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 50 ya
uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China. Uhusiano huo ulitimiza miaka
50, Aprili 26, mwaka huu, siku ambako Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia
ilitimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.
Baada
ya kumaliza ziara yake Beijing, Rais Kikwete atatembelea Jimbo la Jinan ambako
atashuhudia maonyesho rasmi ya kijeshi ya Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa
China la Chinese People’s Liberation Army (PLA) lililoandaliwa rasmi kwa
heshima yake. Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika historia kwa heshima ya namna
hiyo kutolewa kwa kiongozi wa nchi yoyote duniani, nje ya China.
Akiwa
Jimbo la Jinan, Rais Kikwete pia atakutana na viongozi wa Jimbo hilo na pia
atakutana kwa mazungumzo na madaktari wa Kichina ambao wamefanya kazi katika
Tanzania katika miaka 50 iliyopita.
Baada
ya Jimbo la Jinan, Rais Kikwete atakwenda Jimbo la Shenzhen ambako atatembelea makao
makuu ya taasisi na makampuni makubwa ya China ya Shenzhen Economic Zones
Authority, China Merchants Holdings International (CMHI), Huawei na ZTE. Shenzhen
ndiko Watanzania wengi wanaonunua bidhaa kutoka China hufanyia biashara zao.
Mara
ya mwisho, Rais Kikwete alitembelea China mwaka 2008 wakati alipoliwakilisha
Bara la Afrika katika Mkutano wa Kwanza wa China-Afrika katika nafasi yake
wakati huo kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
21
Oktoba,2014
No comments:
Post a Comment