Habari za Punde

Rich Mavoko kupiga shoo ya Instagram Part Zanzibar


NA ANDREW CHALE
MSANII nyota nchini, Richard Martin maalufu Rich Mavoko anatarajiwa kutumbuiza kwenye shoo kali na ya aina yake ya Instagram Part Zanzibar itayofanyika ndani ya Zanzibar Beach hotel, Novemba Mosi  mwaka huu.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo kampuni ya Bond Entertainment, kupitia kwa msemaji wa kampuni hiyo Mackson Madoro  alieleza kuwa kila kitu kipo sawa kwa ajili ya tukio hilo  ambayo mpaka sasa wadau na wapenzi wa burudani wakiwemo wa ndani na nje ya Visiwa hivyo wanaisubiria kwa hamu kubwa.

“Novemba Mosi ambayo itakuwa siku ya Jumamosi, kwa mara ya kwanza, Msanii Rich Mavoko atapiga shoo ya aina yake katika Instagram Part Zanzibar. Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza tokea kwa msanii huyo atoe wimbo wake wa ‘Pacha wangu’  unayotamba kwa sasa” Alisema Madoro.

Kwa upande wake msimamizi wa shoo, Dhamir  Ramz Jr  alieleza kuwa mbali na msanii huyo kutoa shoo pia kutakuwa na wageni maarufu mbalimbali watakaojumuika kwa pamoja na kupiga piucha  kwenye zulia jekundu na watu watakaoudhulia siku hiyo.

“Instagram Part Zanzibar hii si ya kukosa kwani itakuwa na ‘surprise’ za kila aina kutoka kwa watu maarufu watakaopiga picha na wapenzi wa burudani na marafiki watakaojitokeza siku hiyo” alieleza Ramz Jr.

Ramz Jr aliongeza kuwa, shoo hiyo inayotarajiwa kuanzia majira ya mchana  mpaka usiku, ni ya watu wote ambapo ulinzi na usalama umezingatiwa kwa kiwango kikubwa na kuwaomba wajitokez kwa wingi huku kiingilio ikiwa ni sh 10,000 kwa kila mmoja.

Ambapo pia kutakuwa na zawadi  kkutoka kwa wadhamini kwa watu wa mwanzo watakaoingia kwenye siku hiyo ambayo itakuwa ni ya kihistoria kwa kukutana kwa marafiki na kubadilishana mawazo.

Kampuni ya  Bond Entertainment, imekuwa ikijihusisha na masuala ya kuendeleza  tasnia ya sanaa kupitia muziki na wasanii mbalimbali kupitia kazi zao na kuandaa matamasha kwa wasanii wa ndani na nje.

“This event aims to entertain and bring together users of the social network INSTAGRAM with emphasis to creating a conducive environment for all instagrammers to meet and exchange their ideas in social networking and bring awareness with regards to the power of the social media in providing information first hand in all issues including social, political and economic platforms.

It is only a once in a life time event to meet your fellow instagrammers  from diffrent parts of the country. Don't miss it!
The first  attendants will be presented with a special  gift .. exclusively designed for the event. Be there!!”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.