Habari za Punde

TUTASHIRIKIANA NA WAPENDA AMANI KUISAIDIADRC IWE NA AMANI-TANZANIA

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza wakati wa Mkutano wa  Kamati  ya Nne ya Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa iliyokuwa  ikijadili ajenda    kuhusu  tathmini ya jumla ya  Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi zinazochangia wanajeshi wake  katika    operesheni  hizo za ulinzi wa amani.
Sehumu   ya wajumbe wa Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa,  wakifuatilia majadiliano   ya ajenda   kuhusu Operesheni za  Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.



Na MwandishiMaalum, New York
Jamhuri ya Muunganowa Tanzania,imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa yakuwa itaendelea kushirikiana na wapenda amani katika kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa na amani na usalama.

Akichangia majadiliano juu ya ajenda inayohusu tathimini ya jumla ya Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania inafanya hivyo kwa kutambua wajibu wake katika medani ujenzi wa amani ya Kimataifa.

Amesema  pia  kuwa, ni kwa kutambua wajibu huo, ndiyo sababu iliyoifanya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia makubaliano na nchi wanachama wenzie katika SADC na Maziwa Mkuu (ICGLR),kujitolea kupeleka wanajeshi wake huko  DRC ili kuunga mkono juhudi za kuwasaidia wananchi wa DRC kuwa na amani , usalama na maisha yenye uhakika.


Balozi Mwinyi amesema kuwa Tanzania inajivunia kuwa wanajeshi wake  wanaohudumia kupitia FIB  ambayo ni sehemu ya MONUSCO licha ya mazingira magumu na hatari wanayokabiliana nayo wameonyesha umahiri mkubwa ikiwa ni pamoja na kujitoa muhanga maisha ya o kuwalinda raia wasiokuwa na hatia DRC  pamoja na kurejesha amani na usalama.

Kwa sababu hiyo, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, amesema ni vema na haki, kujitoa muhanga huko kwa wanajeshi wanaohudumia FIB kutambuliwa na wapenda amani wote na  vile vile FIB iendelea kupata uungwaji mkono stahili.

Aidha Balozi Mwinyi amesema, kutokana mabadiliko ya mwenendo mzima wa machafuko na vita  katika maeneo mbalimbali Barani Afrika, ikiwa ni pamoja na matishio na kutumik a kwa mbinu za kigaidi na mabomu ya kutengenezwa kienyeji kuna lazimisha kufanyika mabadiliko katika mfumo mzima wa ulinzi wa Amani.

Amesema, mabadiliko hayo yanapelekea Umoja wa Mataifa kulazimika kuidhinisha matumizi ya mamlaka nguvu katika baadhi ya misheni zake kutokana na ukweli kwamba matishio hayo siyo tunihatarisha kwa raia lakini pia   yamekuwa tishio kwa walinzi wa amani.

Kwa sababu hiyo, Tanzania imetaka kuwapoja kwa majadiliano ya kina ndani ya Umoja wa Mataifa kuhusu dhana nzima ya mabadiliko ya mwenendo wa machafukona  vita vinavyoendelea na hatarii nayo wakabili walinzi wa amani pamoja na matumizi ya nguvu kuwa sehemu ya mamlaka nguvu ya misheni nyingi.

“Tunahitaji majadiliano ya kina katika eneo hili,kwa sababu, mwenendo wa machafuko na mbinu za maadui zimebadilika kabisa.Kuna matumizi makubwa ya mbinu za kigaidi na mabomu yanayotengenezwa kienyeji, haya yote na mengine mengi yanabadilisha kabisa historia ya asili ya ulinzi wa amani, amesisiti za Balozi Mwinyi.

Vile vile amesema, majadiliano ya kina yanahitajika katika eneo la matumizi ya teknolojia za kisasa katika operesheni za kulinda amani,zikiwamo ndege za kiuchunguzi zisizoendeshwa na binadamu ( UAS).

Amesemahapanashaka,kama walivyozungu mza wajumbe wengine, matumizi ya teknolojia hizo pamoja na umuhimu wake yanahitaji majadiliano ya kina na makubaliano ya pamoja.

Aidha Balozi Mwinyi amesema,Tanzania inakaribisha nia ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kufanya mapitio ya Operesheni za Ulinzi wa Amani zaUmoja wa Mataifa ( UNPKOs)  na Misheni Maalumu za Kisiasa (SPMs). 

Na ameahidi kuwa Tanzania itashiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Awali akizugumza mwanzoni mwa majadiliano hayo Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO)Bw.Herve Ladsous, amezungumzia mafanikio na changamoto mbalimbali zinazokabili shughuli za ulinzi wa amani.

Amesema katika DRC,Misheni ya Kulinda Amani ( MONUSCO) ambayo ndani yake kuna FIB imeonyesha umahiri na ujasiri mkubwa wa kutokubali kurudi nyuma katika mapambano ya ke dhidi ya makundi ya waasi yenye silaha.

Akasema ushupavu na uhodari huo,licha ya kutoa ulinzi kwa raia pia umefungua fursa mpya ambapo mamlaka za kiutawala za DRC zimeweza kutawala maeneo ambayo huko nyuma yalikuwa yakishikiliwa na kukaliwa na makundi ya waasi.

Katika majadiliano hayo wazumgumzaji wengi wameelezea kusikitishwa kwao na ongezeko la vitendo vya kuvamiwa kwa walinzi wa amani na kusababisha wengi wao kupoteza maisha.

Wakasema, jambo hilo halikubaliki na halipashwi kuendelea kufumbiwa  macho na kwamba ni lazima pafanyike utafiti wa kina wa kwa nini kumekuwa na ongezeko la mashambulizi kwa walinzi wa amani. na wametaka wahusika wa huduma hizo watafutwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Wachangiaji wengine wameshauri na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kupitia DPKO na taasisi nyingine zinazohusika na masuala ya operesheni za ulinzi wa amani, kuangalia upya mazingira ya utendaji kazi ya walinzi hao wa amani, ikiwa ni pamoja na kuwa patia mafunzo zaidi yanayoendana na wakati, vifaa na zana za kisasa na vya uhakika, malipostahili na pia mamlaka zinazotekelezeka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.