Na Zainab Anuwar
Wazazi na walezi wameshauriwa
kutowafanya watoto wao vitega uchumi na kuwafanyisha kazi ngumu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwalimu
Mkuu wa skuli ya msingi Uzini wilaya ya kati, Silima Haji Silima, wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema kitendo cha
kuwatumikisha watoto na kuwalazimisha kufanya kazi kwa ajili ya kuhudumia
familia zao hakikubaliki kwa sababu kinawanyima fursa ya kusoma.
Aidha alisema wazazi wengi
katika shehia hiyo wamekuwa na tabia hiyo jambo ambalo husababisha watoto wengi
kukatisha skuli na kubakia nyumbani.
Alisema ajira za watoto
zinasababishwa na changamoto mbali mbali ikiwemo wazazi kutokuwa na mwamko wa
elimu.
Kwa upande wake Mwajuma Makungu
Is-haka ambae ni miongoni mwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo,
alisema kuna baadhi ya wazazi wanadharau elimu na kuamua kuwatumikisha watoto
wao katika kazi za mikono.
Skuli ya Uzini Msingi ina jumla
ya wanafunzi 534 ambapo wanaume ni 260 na wanawake 274.
No comments:
Post a Comment