Na Kauthar Abdalla
KUNA umuhimu wa kutolewa elimu
ya sheria za kazi kwa wafanyakazi na wanachama wa vyama vya wafanyakazi ili
wajue mahitaji yao ya msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa
Chama cha Huduma za Umma na Afya Zanzibar (ZUPHE) Abdalla Abdulhamid Haji, alipokuwa
akifanya marekebisho ya katiba ya chama hicho katika ukumbi wa Eacrotanal mjini
Unguja.
Alisema kwa kuwa taasisi hiyo imelenga zaidi kutoa
huduma hivyo ipo haja kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa taasisi mbali mbali
kujua sheria za kazi ili waweze kutetea maslahi yao kwa misingi inayotakiwa.
Aidha alisema katiba
iliyokuwepo ya mwaka 2008 ina upungufu mwingi unaomnyima haki wanachama hivyo
kuna haja ya kufanyiwa marekebisho.
Alisema lengo la kurekebisha
katiba ya chama hicho ni moja ya hatua za kutatua migogoro kati ya muajiri na
muajiriwa ili kupatikana haki na fursa stahiki pande zote mbili.
Nae Mjumbe wa chama hicho,Rehani
Haji Suleimani, alisema katika marekebisho ya katiba hiyo ni vyema chama kifuatilie
na kuhakikisha shughuli mbali mbali zilizolengwa zinatekelezwa.
No comments:
Post a Comment