Habari za Punde

Balozi Seif azindua ujenzi wa tawi la CCM Milimuni, Aweka jiwe la msingi Ofisi ya Polisi Jamii Chambani

 
MJUMBE wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe: Hemed Suleiman Abdalla, wakati alipowasili katika Ujenzi wa Tawi la CCM cha Milimuni Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiweka sawa tufali katika tawi la CCM Milimuni jimbo la mkanyageni Wilaya YA Mkoani, kuashiria uzinduzi wa tawi hilo, kushoto ni mkuu wa Wilaya hiyo Mhe: Hemed Suleima Abdalla.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiweka utogo kuashiria kuyafunga matufali katika Tawi la CCM Milimuni,  wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa tawi hilo, Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiwaonyesha wanaCCM katiba iliyopendekezwa ambayo wanapaswa kuipigia kura ya ndio, mara baada ya kuzindua ujenzi wa Tawi la CCM milimuni jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi ofisi ya Polisi Jamii shehia ya Chambani, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akikaguwa ujenzi wa ofisi ya Polisi Jamii Shehia ya Chambani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.