Habari za Punde

Elimu kwanza ndio mbiu ya Ujumbe wa Makunduchi Wakiwa Ziarani Nchini Sweden


Manispaa ya Sundsvall, Sweden yapeperusha bendera ya Zanzibar kuonyesha heshima yao kwa ujumbe wa wadi za Makunduchi wakati ndugu Magnus Braxenholm akitoa maelezo kuhusu muundo wa Manispaa ya
Sundsvall pamoja na kazi zake za kila siku. Maelezo hayo yalitolewa kabla ndugu Hafifth bin Ameir (senior citizen of Makunduchi) hajahutubia Baraza la Manispaa (Sundsvall Municipal Assembly) lenye wajumbe zaidi ya 100.


Mtaalamu wa elimu kutoka Manispaa ya Sundsvall ndugu Roy Resare akitoa maelezo kwa ujumbe wa Wadi za Makunduchi (hawapo kwenye picha) kuhusu mikakati ya Manispaa kuwa na Skuli bora nchini Sweden na duniani kote ifikapo mwaka 2021
Ujumbe wa wadi za Makuduchi na bendera ya Zanzibar katika picha ya pamoja na wenyeji wao ndanibya Jengo la baraza la Manispaa (Sundsvall Municipal Assembly). Kutoka kushoto mwalimu mkuu wa skuli ya Makunduchi, Kinore; ndugu Sweden; diwani Zawadi Hamdu; ndugu Mohd Simba; ndugu Mohamed Muombwa na ndugu Hafifth bin Ameir (senior citizen of Makunduchi)
Ujumbe wa wadi za Makunduchi wapata heshima ya kuhudhuria na kuhutubia ndani ya kikao cha Baraza la Manispaa ya Sundsvall (Sunesvall Municipal Assembly) Kwenye picha ndugu Hafifh bin Ameir (senior citizen of Makunduchi) akihutubia kwenye baraza lenye wajumbe zaidi ya 100. Katika hutuba yake ameelezea umuhimu wa mashirikiano kati ya Makunduchi na Manispaa ya Sundsvall. Huu ulikuwa ni mkakati wa wadi za Makunduchi kuwashawishi wajumbe wa Baraza kupitisha kwa kishindo mashirikiano ya sekta ya elimu.
Miongoni mwa mikakati ya wadi za Makunduchi ni kuitangaza Zanzibar kiutalii pamoja na biashara ya wanawake wa Makunduchi. Diwani Zawadi Hamdu akimkabidhi zawadi ya kipochi cha ukili bi. Christin ambaye ni mratibu wa mashirikiano.
"Ahaaa unapendeza bi Christin!"Hayo ndiyo maneno aliyonena diwani Zawadi baada ya kumaliza upambaji

3 comments:

  1. Ahsanteni kwa kupeperusha bendera yetu naiona hapo na ndivyo inavyotakiwa

    ReplyDelete
  2. Mambo yanakwenda vyema kaka kumena Bendera vyo juu ya meza na kutulwa kati

    ReplyDelete
  3. sasa unaona kama huyo sefu ni garasa yeye kaenda nje ya nchi anazungumza na watembezaji watalii hebu angalia hao kutoka kae wametinga ndani ya kikao cha Baraza la Manispaa ya Sundsvall (Sunesvall Municipal Assembly) ambalo lina maamuzi yote ya manispaa yao lkn ww unazungumza na wateja duuu kwisha maaalimm hakiiiii haki sawa kwa nani kwa watembeza wataliii. Hongereni watu wa kwetu Kae maendeleo mbele waacheni hao mabishooo kina maalim wazungumze na matejan tuuu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.