Habari za Punde

Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi Waendelea na Ziara Yake Nchi Sweden.

Mwanasiasa mpenda maendeleo ndugu Mohd Simba baada ya kufanya mazungumzo yatakayopelekea wanasiasa vijana kutoka Makunduchi kubadilishana ziara na wanasiasa vijana wa Manispaa ya Sundsvall. Ziara hizi zitatoa mafunzo kwa wanasiasa wachanga wa Makunduchi kuwa na siasa za kuleta maendeleo badala ya kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi. Aidha ziara hizi zitawafunda vijana wetu demokrasia halisi, uwajibikazi pamoja na dhana halisi ya jinsi ya kufuatilia utendaji katika ngazi ya serikali za mitaa.
Ujumbe wa wadi za Makunduchi wakutana na balozi wa Tanzania nchini Sweden ndugu Dora M Msechu hapo ubalozini. Katika picha kutoka kulia ni Dr. Mohamed Mwinyi, ndugu Mohamed Muombwa, ndugu Sweden, ndugu Mohd Simba na ndugu Hafifth bin Ameir (Senior Citizen of Makunduchi) kutoka kushoto msaidizi wa balozi ndugu Jackob, ndugu Trevor Fisher, mwalimu Kinore na diwani Zawadi
Ndugu Hafifth bin Ameir (senior citizen of Makunduchi) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika ubalozi wa Tanzania nchini Sweden. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.