Habari za Punde

HIFADHI YA MSITU WA JOZANI

Ni   umbali  wa  kilomita  35 kutoka kusini  mashariki  mwa  Unguja  ambapo  utakuta  msitu wa hifadhi wenye kupakana na ghuba ya Chwaka.
            Hifadhi  hiyo  imejumuisha vijiji tisa  vikiwemo Pete , Kitogani ,Ukongoroni  chwaka ,Charawe ,Unguja ukuu, Michamvi na Cheju .
      Taratibu  tunaingia  katika  hifadhi  ya  msitu  huo  ghafla  tunaona  kuna  vitu  vya aina mbali mbali vya  ajabu  ambayo  ni  vivutio  vikubwa   vya  utalii ambao huwavutia  watu  kutoka  kila  kona  ya  Dunia.
       Vivutio hivyo vimegawika katika sehemu tatu vikiwemo daraja la mikoko,sehemu Kima punju na Msitu.
    “Msitu huo una miti   ya aina mbali mbali kama mitondoo, mivinje , mikaratusi miti mafuta, mikonge, mikangara shamba na mingi mingineyo, ambayo ina urefu wa ajabu na kushonana juu yake jambo ambalo hufanya jua lisionekane katika eneo hilo,”Alisema ndugu Ali Khamis Moh”d ambae ni mkuu wa hifadhi  ya msitu wa  Jozani,alipoanza simulizi juu ya hifadhi hiyo.

     Alisema kuna baadhi ya miti ni dawa na hii mara nyingi hupatikana katika msitu huu wa Jozani kama  vile Misiliza ambayo hutumika kama dawa ya kuondoa minyoo tumboni.
     “Na baadhi ya miti mingine hutumika katika kutengenezea mafuta mfano mti wa mkunazi,”aliongeza  mkuu wa Hifadhi  hiyo.
      Pia alisema  katika msitu wa hifadhi wa Jozani kuna wanyama adimu ambao hawapatikani katika hifadhi nyengine yoyote kwa mfano  chura wa Jozani,Chuwi wa Zanzibar,Jongoo wa Jozani,Kima Punju,Paa nunga na wingineo  wingi.
    “ Hata hivyo  katika Wanyama wote hao Kimapunju ndio kivutio kikuu cha watalii kutokana na rangi yake ,umbile na tabia yao ya kuishi ujamaa kama Binaadamu,”alieleza ndugu Ali.
      Alizungumzia kidogo juu ya Kima punju alisema huishi na kufuatana kwa makundi na kila kundi huwa mna dume mmoja na kamwe hakubali kuliacha kundi hilo kuingiliwa na dume mwengine hadi kufa kwake.
       Vile vile alisema Kima punju hupendelea sana kula majani  machanga ya miti kama vilele vya mipera na majani ya mikungu ambayo ndio hupendelea kula zaidi jambo ambalo husababisha mikungu yote ya Jozani kutokuwa na majani kabisa kwani  yakichipua tu huliwa.
     Alisema wanyama hao hula maganda ya matunda  kama vile Embe,Mapera na makoroma ya nazi na hawali kabisa matunda yenye sukari  kama vile Embe mbivu ,Ndizi mbivu  kutokana na matumbo yao kushindwa kusaga vitu vya sukari(insuline  hormone).
     “ Kima punju hula makaa  meusi kama ni tiba ya maradhi mbali mbali yanayowasumbua na ni kinga  ya maradhi yao,” alifahamisha.

 “ Vile vile Kima punju hukaa  zaidi ya miezi mitano bila ya kunywa maji kutokana na vyakula wanavyokula si vya kunywesha maji, kwani mara nyingi hula vyakula vyenye ukafu vikiwemo vilele vya  majani machanga,” alifafanua  ndugu Ali.
       Licha ya kuwa Kima punju kuwa  ni kivutio kikuu cha watalii pia Chura wa Jozani anaepatikana katika Bwawa la maji baridi la Mwanjoza nae ni kivutio kikubwa kutokana na kuwa ni mnyama pekee anaepatikana Jozani tu .
      “ Pia aliendelea kwa kusema  kila baada ya miaka kumi na tano (15) huvumbua mnyama au mti mpya  katika hifadhi hiyo, kwa miaka kumi na tano ( 15) iliyopita tulivumbua Chura wa Jozani katika Bwawa la Mwanjoza”,alisema mkuu huyo wa Hifadhi.
      Alisema  Bwawa la Mwanjoza ni Bwawa la ajabu lililopo katikati ya msitu wa Jozani, kutokana na kuwa na vitu vya ajabu kama miti iliyoota chini  ya maji na mizizi yake kutokeza juu ya Bwawa,Miti iliyoota juu ya miti mwenzao  na mengine iliyoota juu ya maji kama mayungi yungi yenye maua ya kupendeza .
         “ Kwa kweli  Bwawa la Mwajoza linaongeza hadhi ya uzuri wa  msitu wa hifadhi wa Jozani  kwani licha miti hiyo pia kuna chura wa Jozani alivumbuliwa katika Bwawa hilo,”aliongeza.

         Baada ya kuondoka katika Bwawa la Mwajoza tulielekea katika Daraja la Mikoko ambapo tulichukuwa dakika 40 kutembea kwa miguu .
         Njiani tuliona vipepeo aina mbali mbali kama Dadanesi nawengine wengi wenye rangi ya kupendeza kama  Karasisi ambae hupatikana Zanzibar tu.
         Tukiwa tunaendelea na safari ghafla tuliona Bango la mradi wa Kasa tulipouliza alisema kuwa “huo ni mradi wa Tassaf  na hausiani kabisa na hifadhi ya Msitu wa Jozani,”alifafanua ndugu Ali.
          Baada ya dakika kumi tulifanikiwa kufika katika  Daraja la Mikoko ambapo huko kuliwa na uzuri wa ajabu kutokana na Miti hiyo ya Mikoko kushonana na kunawiri vizuri katika maji chumvi yalioko chini ya Daraja hilo la mbao.
          Mikoko hiyo ipo ya aina tatu : mikoko meupe,mikoko meusi na  mikoko mekundu(magando) ambayo ndio inaengeza hadhi ya Daraja hilo kutokana na miti hiyo kuwa na matawi mengi na mizizi yake huchomo juu ya ardhi kwa kiasi kikubwa jambao ambalo huwezi kuwamini kama mizizi waweza hisi nayo ni jumla ya matawi ya miti hiyo.
     Nae Mkuu wa kitengo cha Utalii ndugu Salum Ramadhani alisema kuwa Msitu wa Jozani ni miongoni mwa sekta muhimu ya utalii yenye kuingiza fedha nyingi  kwa serikali,kutokana na kuwa na vivutio vya kila namna katika hifadhi hiyo.


        “  Kila mwaka tunapokea  wageni kutoka  sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi takribani 25,000 kwa mwaka  ambao huchangia  zaidi ya Tsh milioni 400,” alifafanua ndugu Salum Ramadhani.
     “  Aidha  alisema    wageni wengi  kutoka nchi za  Ujerumani, Uingereza, Marekani,Ufaransa na Italia,    Wageni wengi zaidi hutoka utaliana   kutokana na kuwa na usafiri wa moja kwa moja,”  aliendelea  kueleza ndugu Salum.
    Aliendelea kwa kusema kuwa mapato yanayopatikana  kutokana na uingiaji wa wagani hao hugawiwa  katika mafungu mawili alifahamisha kuwa,Fungu la kwanza ni la serikali ambalo ni asilimia 50 na fungu la pili ni la wanavijiji ambalo nalo ni asilimia 50  kwa  wanavijiji waliozunguuka hifadhi hiyo.
     “  Hii ni    Kutokana na kuharibiwa  mazao yao  na wanyama waharibifu kama kima,Nguruwe pamoja na wanyama wengine na kukosa maeneo ya kutosha kwa  ajili ya  kilimo  kikiwemo kijiji cha Pete kutokana na eneo kubwa la ardhi  yao kuingia ndani ya hifadhi hiyo,”  alifafanua ndugu Salum.1/29/2015
     Nae mmoja  miongoni mwa wanavijiji hao ndugu Moh’d Ali Mchobwa alisema kuwa  kwa sasa wanafaidika na hifadhi  hiyo kwa kupokea fedha kutoka  katika mgao wa kila mwaka na kufanikiwa kujenga skuli kwa maendeleo ya watoto wao.
      “Zamani walikuwa watoto wanapata tabu sana maana wanatembea masafa marefu kufuata Elimu kwenye vijiji vya mbali kama vile Kitogani na Muyuni” .alisema ndugu Mchobwa.
      Hata hivyo ,mkuu wa hifadhi hiyo alisema, licha ya Hifadhi hiyo kuwa na faida nyingi pia hukabilwa na changamoto mbali mbali zikiwemo kuungua moto   kila baada ya mwaka   kutokana na mkusanyiko wa majani mengi  ambayo  hupelekea kuwaka moto wenyewe.
       Aidha sababu nyengine zinazopelekea   msitu huo kuungua moto  ni uvunaji haramu wa Asali pamoja na wasasi ambao hutafuta wanyama   kama nguruwe na Paa kwa ajili ya  kitoweo,Hivyo kutokana na kazi hiyo ngumu ya uwindaji ambayo hufanywa wakati wa usiku  baadhi ya wasasi huvuta sigara na vipande hutupwa na kusababisha mlipuko wa moto.
         Pia aliendelea kwa kusema  kuwa wanao  walinzi mbali mbali lakini bado suala hilo linakuwa guumu kutokana na ukubwa wa  Hifadhi hiyo.
           Alisema  kutokea kwa moto husababisha  kukimbia kwa wanyama kama vile paa  na hata wanyama wengine ambao ni wazito kukimbia hufa  mfano Chatu, Nyoka na hata wadudu wadogo wadogo wakiwemo Jongoo wa Jozani pamoja na miti ya asili kutoweka.
          Hifadhi ya Jozani si hifadhi ya  kuoteshwa bali ya asili  na rasilimali zilizomo zimehifadhiwa tangu zamani.
          Katika eneo la Jozani palikuwa na mtawala aliyejulikana kwa jina la JOSHI, ambae alikuwa mfanya biashara wa kihindi.Mfanya biashara huyo  alikuw
a akiishi eneo hilo mnamo mwaka 1930 hadi kufikia 1996 msitu huu ulirejeshwa mikononi mwa wanavijiji ilikuwa ni hatua ya kwanza kuhifadhi na kuulinda.

     Mfanya biashara huyo ambae alikuwa akiishi karibu na Bwawa la Mwajoza   ambalo alikuwa akitumia kwa shughuli  mbali mbali za kila siku, Hivyo  jina la  mtawala Joshi  na eneo alilokuwa akiishi Mwajoza ikapelekea kupatikana kwa jina la Jozani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.