Habari za Punde

Mafunzo ya usafi wa mazingira, Wete

 
WASHIRIKI wa mafunzo wa siku tatu juu ya usafi wa mazingira, yalioandaliwa na Jumuia ya Vijana Jimbo la Kojani ‘KOYMOCC’ wilaya ya Wete Pemba na kufanyika skuli ya kisiwa cha Kojani, ambapo tayari hali ya usafi wa mazingira kisiwani humo imeimarika baada ya kumalizika kwa mradi huo wa mwaka mmoja, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 MSHIRIKI wa mafunzo ya usafi wa mazingira kutoka Kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete Pemba Ali Hamad Dau, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo yalioandaliwa na Jumuia ya Vijana Jimbo la Kojani ‘KOYMOCC’ ambapo mradi huo wa mwaka mmoja, tayari wananchi zaidi ya 700 wameshapewa taaluma ya usafi wa mazingira, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MWENYEKITI wa Jumuia ya Vijana  Jimbo la Kojani ‘KOYMOCC’ wilaya ya wete Pemba, Bakar Suleiman Juma, akielezea mafanikio ya mradi wa usafi wa mazingira, uliokuwa chini ya KOYMOCC, ambapo umekiimarisha kiusafi kisiwa cha Kojani, sambamba na kuwapa elimu hiyo wananchi zaidi ya 700 wa shehia za Kojani na Mpambani, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.