Habari za Punde

Mawaziri wa Afya wa SMT na SMZ wakutana na watanzania Ujerumani


Waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Bw.Seif Rashid na Waziri wa afya wa Zanzibar Mhe. Rashid Seif Suleiman, Siku ya Jumapili 25 Januari 2015 walikutana na kuongea na baadhi ya watanzania waishio nchini ujerumani katika hoteli ya Martim Hotel mjini Berlin.
 
Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Bw.Philip Malmo.
 
Katika mkutano huo mawaziri hao wote walielezea jinsi Wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila mtanzania atatanufaika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao.
 
Watanzania waishio Ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo pia mawaziri wamewataka watanzania waishio ughaibuni kuchangia kuwekeza katika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi.
 
Mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo

1 comment:

  1. Mwandishi unapotosha jamii kwa makusudi au no mbumbumbu Wa mambo. Hakuna Waziri Wa Afya na Ustawi Wa Jamii Wa Jamhuri ya Muungano hapa Tanzania kwani Afya na Ustawi Wa Jamii si mambo ya Muungano. Tafuta title yake inayostahiki umpe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.