Habari za Punde

Maziko Mshauri wa Rais Mambo ya Utalii Zanzibar Marehemu Issa Ahmed Othman

Ndege ya Shirika la Ndege ya Oman Air ilochukuwa mwili wa marehemu Mhe Issa Ahmeid Othman aliyefariki Nchi India akiwa katika matibabu na mauti kumkuta huko Mwenyezimungu amjalie safari ilionyoka Amin.ikiwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo mchano. 
Wananchi wakiungana na Ndugu na Jamaa katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuupokea mwili wa aliyekuwa Mshauri wa Rais Utalii marehemu Issa Ahmeid Othman ukitokea Nchini India alikokwenda kwa matibabu hivi karibuni na mauti kumkuta huko Mwenyezi Mungu ampe kauli thabiti Amani.  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume wakiwa nyumbani kwa marehemu walipofika kuwafariji wafiwa mazizini Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Ameir Kificho na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji wakijumuika na wanafamilia katika kumuombea dua marehemu nyumnbani kwake mazizini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Karume na Viongozi wengine wakitoka kutoa mkono wa pole kwa Wafiwa na kuelekea Msikitini kwa ajili kuusalia mwili wa aliyekuwa Mshauri wa Rais Utali Zanzibar Marehemu Issa Ahmeid Othman.

Wananchi wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa mwili wa aliyekuwa Mshauri wa Rais Utalii Zanzibar wakiingia katika Masjid Mahfuodha Mazizini Unguja kwa ajili ya kuusalia kwa mazishi kijiji kwake Kianga Unguja.

Viongozi wa Serekali na Wananchi wakiitikia dua ya kuhitimisha hitma baada ya kisoma cha hitma kumsomea marehemu Issa Ahmeid Othman. 
Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar Mwalimu Siasa akitowa mawaidha kabla ya kumsalia marehemu Issa Ahmeid Othman. 
Watoto wa marehemu Issa Ahmeid Othman wakiwa katika masjidi Mahfoudha Mazizini kujumuika na Waumini wa dini ya kiislamu kumuombea mzazi wao.
Maalim Abdallah Issa akitowa shukrani kwa niaba ya Wafiwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa Ibada ya Sala ya maiti kumalizika. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume (kulia) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumswalia  aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Masjid Mahfoudh Mazizini, Marehemu alifariki juzi Nchini India na kuzikwa leo Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika Sala ya Maiti kuusalia mwili wa marehemu Issa Ahmeid Othman katika Masjid Mahfuodha Mazizini Unguja.
Viongozi wa Serekali na Wananchi wakiinua jeneza lenye mwili wa marehemu Issa Ahmeid Othman baada ya kuusalia katika masjid Mahafoudha Mazizini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakijumuika na Wananchi mbalimbali katika mazishi ya aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein katika makaburi ya Kijiji kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Wananchi wa Zanzibar wakishiriki mazishi ya aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Zanzibar Mambo ya Utalii Marehemu Issa Ahmeid Othman, yaliofanyika katika kijiji cha kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akijumuika na Wananchi katika maziko ya aliyekuwa Msahauri wake mambo ya Utalii marehemu Issa Ahmeid Othman, akiweka mchanga katika kaburi.maziko hayo yamefanyika kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Zanzibar Masuala ya Utalii Zanzibar marehemu Issa Ahmeid Othman, aliyezikwa kijiji Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. 
Wananchi kutoka nje ya Zanzibar na Zanzibar wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Issa Ahmeid Othman baada ya mazishi yake yaliofanyika katika kijiji cha kianga nje kidogo ya mji wa Unguja Wilaya ya Magharibi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.