Habari za Punde

Mshindi wa Kwanza wa Promosheni ya Zantel Kwangua Ushinda Ajishindia Friji Zenj.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu ya Zantel Ndg Mohammed Mussa Khamis (Baucha) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa Premosheni ya Zantel ya kwagua kadi ya shilingi mia moja na kutia fedha kutumia Mimina kiasi cha shilingi 1000/= ili kushiriki promosheni hiyo na kujishindia zawadi kama zinavyoonekana katika tangazo la hapo juu. Mshinda wa kwanza Bi Mwanaid Rajab Silima akichukuliwa zawadi yake na Mumewe Ndg. Hassan Abdallah akikabidhiwa zawadi hiyo katika Ofisi za Zantel Mlandege Zanzibar.
Meneja Masoko wa Zantel Ndg Mohammed Mussa Khamis akimpongeza mshindi wa kwanza wa Promosheni ya kuingiza kadi ya shilingi 1000/- na kwa kutumia Mimina unaweza kujishindia zawadi za Friji, Simu ya Samsung na muda wa maongezi wa shilingi 10,000/=.anayeshihudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Zatel Bi Progres Chisenga, makabidhiano hayo yamefanyika katika Afisi ya Zantel Mlandege jengo la Muzammil.
Meneja Masoko wa Zantel Ndg Mohammed Mussa Khamis akizungumza na mwandishi wa habari kuhusiana na kushiriki katika promosheni hiyo inayowashirikisha Wananchi walioko  Zanzibar tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.