Habari za Punde

Uzinduzi wa Sherehe za CCM Miaka 38 Kisiwani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana na Nainu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Bakari Mshindo (wa tatu kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) wakipiga makofi ulipopigwa wimbo wa Chama kumpokea Dk.Shein alipofika kuzindua Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo,

Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar walipokuwa wakiwasalimia WanaCCM wa Mikoa miwili ya Pemba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein 
Vijana wa Chipukizi wa CCM Kisiwani Pemba wakiimba Wimbo Maalum wa kuzaliwa CCM wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani)
Picha ya Muasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikinyanyuliwa juu wakati Wimbo maalum ukiimbwa na Vijana wa Chipukizi walioshiriki halaiki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akisema machache na kumkaribisha katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana ili awaslimie wananchi wa Mikoa ya Pemba wakati wa  uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
Baadhi ya WanaCCM wa Mikoa miwili ya Kisiwa cha Pemba wakiwa katika Uzinduzi wa Mkutano Maalum wa Sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba uliohutubiwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana baada ya kumalizika kwa Mkutano wa maadhimisho ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.