Na Kija Elias, Moshi
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dk Jakaya Mrisho Kikwete,
ameagiza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro
chini ya mkuu wake wa mkoa, Leonidas Gama, kutenga maeneo ya kutosha kwa ajili
ya uwekezaji ikiwamo viwanda vitakavyowezesha
kuwe`po vitega uchumi vingi katika mkoa
huo.
Alitoa ushauri huo mkoani Kilimanjaro katika hafla ya uzinduzi wa jengo la
kisasa la kitega uchuni ambalo limejengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,NSSF, na
kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 64 hadi kukamilika kwake.
Alisema nchi yeyote duniani haiwezi kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi
bila viongozi kukaa pamoja kuweka mazingira ambayo yatasaidia kuinua uchumi wa
mkoa huo na maeneo husika.
Aliwataka viongozi hao kutengeneza mazingira wezeshi katika kutenga
maeneo ya uwekezaji yatakayokuwa rafiki kwa wawekezaji ambao watakuwa tayari
kuwekeza katika mkoa huo tofauti na sasa ambako wawekezaji wengi wamekuwa
wakikimbilia katika mkoa jirani wa Arusha.
Alisema uwepo kwa jengo hilo la kisasa ambalo limekuwa kivutio kikibwa
katika mji wa Moshi unaotarajiwa kuwa jijiji hivi karibuni,kutawavutia watu
wengi kuendesha shughuli zao za kibiashara pamoja na mikutano ya kimataifa.
Katika hatua nyingine,Rais Kikwete aliwataka wanasiasa kuacha kutumia
ubabe kwa kupinga shughuli za maendeleo
ambazo zimekuwa zikitekelezwa na mkoa huku akimlenga Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Moshi,Jaffari Michael.
Alimtaka Meya huyo kuwa mstari wa mbele kuunga mkono shughuli za
maendeleo badala ya kuwa mpinga maendeleo namba moja na kuacha mbwembwe za
kisiasa ambazo haziwezi kuleta maendeleo kwa wakazi mji wa Moshi.
Awali akimkaribisha Rais Kikwete, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama,
alisema uwepo wa jengo hilo utachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumia wa
mkoa, na kwamba watilii wanaofika na kutembelea mlima Kilimanjaro watafika
katika jengo hilo na kujipatia mahitaji yao kabla ya kupanda mlima huo.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo, Jaffari Michael, alisema tayari
halmashauri hiyo imekwisha kutenga maeneo ambayo yatatumika kama vitega uchumi
vya mkoa.
No comments:
Post a Comment