Habari za Punde

Ujumbe wa manispaa ya Sundsvall kutoka Sweden waendelea na ziara jimbo la Makunduchi


 
Mwalimu Hafidh, senior citizen wa Makunduchi, akitoa maelezo kwa ujumbe wa Manispaa ya Sundsvall juu ya ujenzi wa Sustainable Center of Learning ya Makunduchi itakayojengwa kigaeni Makunduchi. Kituo hiki kinategemewa kutoa elimu katika nyanja mbali mbali kama biashara, ufugaji wa nyuki, elimu ya kompyuta n.k. Kutoka kushoto kwenye picha ni bi. Christin Stromberg, ndugu Sweden na ndugu Trevor Fisher
 Walimu wakuu na wasaidizi wao na wajumbe wa kamati ya wadi za Makunduchi wakimsikiliza bi. Christin, hayupo kwenye picha, juu ya mradi wa miaka 3 ya kuwaongezea uwezo walimu. Katika mkutano huu uliofanyika Skuli ya Makunduchi walimu walipata fursa ya kutoa changamoto zao.
 Bi. Christin Stromberg akitoa maelezo kwa walimu wakuu na wajumbe wa kamati ya wadi za Makunduchi juu ya mradi utakaowajengea uwezo walimu wakuu na wasaidizi wao kutoka Skuli 6 za Makunduchi. Mradi huu utakapotekelezwa utatoa mafunzo ya ndani na nje ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya wadi za Makunduchi, mwalimu Mwita Masemo akipokea ramani ya jengo la Makumbusho kutoka kwa mratibu wa manispaa ya Sundsvall bi. Christin linalotegemewa kujengwa na kamati huko Makunduchi. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.