Na Abdi Suleiman, Pemba
JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini
Pemba, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Makame Ali Suleiman
(Dude), aliyeuawa katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Juma Yussuf Ali, alisema marehemu
aliokotwa chini ya mnazi ambao unagemwa pombe, hali inayoonesha kulikuwepo
ugomvi wa kuwania pombe baina ya marehemu na watu waliofanya mauaji hayo.
Alisema baada ya upelelezi kukamilika,
watuhumiwa watafikishwa katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo
wake.
Tukio hilo lililotokea usiku
wa kuamkia Febuari 6 katika bonde la Oka Kangani wilaya ya Mkoani, baada ya
wananchi waliokuwa wakipita njiani kuona mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa.
Marehemu alikatwa bega la
kushoto na kutolewa lote, kuharibiwa sehemu za usoni na macho, kupasuliwa
kichwani, kukatwa masikio na kukatwa vidole.
Aidha alisema mtu mmoja
anashikiliwa baada ya kuvamia nyumba moja katika kijiji cha Pujini na tayari
ameshafikishwa mahakamani.
Kamanda huyo alimtaja
mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Fesha, ambaye ana rekodi nyingi za matukio ya
uhalifu.
No comments:
Post a Comment